Tuesday, 13 June 2017

BREAKING NEWS: TAARIFA KWA UMMA JKT IMEONGEZA ORODHA YA MAJINA YA VIJANA WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MEI 2017 KWA AJILI YA KUHUDHURIA MAFUNZO YA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2017

ad300
Advertisement
TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linapenda kuutaarifu umma kuwa limeongeza majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwezi Mei 2017 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.

Vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 13 Juni 2017 hadi tarehe 20 Juni 2017.

Mkuu wa JKT, kwa mara nyingine tena, anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

Orodha kamili ya majina ya vijana hao walioongezwa, maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT 


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 13 Juni 2017

Share This
Previous Post
Next Post

FURSA AJIRA Is is an East Africa site which announcing, publishing job vacancies everyday from the government portals, recruiters agencies, organizations, companies and institutions to those jobless people. Get your dream job by visiting this site everyday or just install Fursa Ajira App

0 comments: